Matangazo ya Usharika tarehe 6/11/2022

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 06 NOVEMBA, 2022    

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

SISI NI WENYEJI WA MBINGUNI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 30/10/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

Azania Front Cathedral Yaadhimisha Sikukuu ya Mavuno 2022

Siku ya Jumapili, tarehe 30/10/2022, Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azaniafront Cathedral ulifanya maadhimisho ya sikukuu ya mavuno pamoja na sikukuu ya matengenezo ya kanisa. Sikukuu ya mavuno hufanyika kila mwaka ili kutoa fursa kwa washarika kumtolea Mungu sehemu ya matunda au mavuno ya kazi wanazozifanya.

Ibada ya kusherehekea sikukuu hii ya mavuno kwa mwaka 2022 imefanyika katika viwanja vya usharika wa Kanisa Kuu Azania Front huku ikihudhuiriwa na mamia ya washarika waliojitokeza kwa wingi wakiwa na mavuno yao tayari kwa kumtolea Mungu.