Kwaya Kuu yazindua DVD

Jumapili ya tarehe 24/03/2019 Kwaya Kuu ya Kanisa Kuu la Azania Front ili fanya Uzinduzi wa Kanda yake ya Kwanza ya DVD yenye nyimbo 10 yenye jina la SIKU MOJA ILIYOBADILI MAISHA YANGU. Uzinduzi huo ulifanywa na Mch Charles Mzinga kwa niaba ya Baba Askofu Alex Gehazi Malasusa. Kwaya hii imeshatoa kanda za Audio/CD tisa. DVD hii imetokana na kanda ya CD ya tisa yenye jina hilo hilo. Kwaya hii ilianza mwaka 1950 na Ina miaka 69 sasa. Mgeni Maalumu katika Uzinduzi huo alikuwa Mhe Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.