Date: 
28-02-2023
Reading: 
2Wakorintho 6:1-10

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi tarehe 28.02.2023

2 Wakorintho 6:1-10

1 Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.

2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)

3 Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe;

4 bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;

5 katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga;

6 katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki;

7 katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;

8 kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli;

9 kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa;

10 kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.

Tukimtegemea Bwana tutashinda majaribu;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Kanisa la Korintho kutoipokea neema ya Mungu bure. Anawaita kuwajibika wakitimiza wajibu wao katika utume walioitiwa, ili utumishi wao usilaumiwe. Mtume Paulo anawasisiza watu wa Korintho kujipatia sifa njema kama watumishi wa Mungu walioitwa kutumika shambani mwake. 

Kuwajibika katika utume wetu kunakuwa katika njia sahihi pale tunapomtegemea Bwana. Bwana hutuongoza jinsi ya kuenenda kwa usahihi katika kazi yake, hivyo kumtegemea ni muhimu sana. Tukumbuke kutubu dhambi zetu kwa Bwana tukimtegemea wakati wote ili utume wetu uwe mwema. Siku njema.

Heri Buberwa