Date: 
28-05-2019
Reading: 
1 Kings 18:36-40 (1 Wafalme 18:36-40)

TUESDAY 28TH MAY 2019 MORNING                                          

1 Kings 18:36-40 New International Version (NIV)

36 At the time of sacrifice, the prophet Elijah stepped forward and prayed: “Lord, the God of Abraham, Isaac and Israel, let it be known today that you are God in Israel and that I am your servant and have done all these things at your command. 37 Answer me, Lord, answer me, so these people will know that you, Lord, are God, and that you are turning their hearts back again.”

38 Then the fire of the Lord fell and burned up the sacrifice, the wood, the stones and the soil, and also licked up the water in the trench.

39 When all the people saw this, they fell prostrate and cried, “The Lord—he is God! The Lord—he is God!”

40 Then Elijah commanded them, “Seize the prophets of Baal. Don’t let anyone get away!” They seized them, and Elijah had them brought down to the Kishon Valley and slaughtered there.

This was a contest to prove who is the true God.  Elijah wanted to show that our God is true and not like the idols whom other nations worshipped. Elijah called upon God to answer His prayer and to send fire to burn up the sacrifice.

God answered His prayer and the people believed. 

Let us pray for God’s name to be honoured and for people to come to faith in Him.   


JUMANNE TAREHE 28 MEI 2019 ASUBUHI                           

1  WAFALME 18:36-40

36 Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. 
37 Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. 
38 Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. 
39 Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu. 
40 Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko. 
 

Hapa kulikuwa na mashindano kuonyesha Mungu wa kweli ni yupi. Eliya alitaka kuonyesha kwamba Mungu wetu ni Mungu wa kweli mwenye nguvu na mamlaka siyo kama Baali na sanamu wengine.

Eliya alimwomba Mungu aonyeshe uwezo wake kwa kutuma moto kuteketeza sadaka. Mungu alifanya hivyo. Watu wameona na kumwamini Mungu wa kweli.

Mwombe Mungu atukuzwe katika maisha yako na watu wavutiwe kumwamini.