Event Date: 
14-03-2022

Wanawake usharikani walishiriki katika kuongoza ibada ya Kwaresma iliyofanyika siku ya Jumatano tarehe 9/3/2022, ibada hiyo ilifanyika kwa kutumia kitabu maalum cha maombi ya dunia cha mwaka huu, ambapo ibada kuu ya maombi hayo ilifanyika siku ya Ijumaa tarehe 4/3/2022 ambayo yalishirikisha wanawake wote duniani.

Ibada hii ya usharikani iliongozwa na Mama Veronica Kileo na mahubiri yalitolewa na Bibi Jacqueline Swai, neno kuu katika ibada hii ya maombi lilitoka katika kitabu cha nabii Yeremia 29:11.

Wanawake walishiriki katika ibada ya maombi usharikani wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mama Askofu Erica Malasusa.

-----------------------------------------------------

Ripoti hii imeandaliwa na Jane Mhina