Event Date: 
14-03-2022

Viongozi wa Umoja wa wanawake usharikani, wakiongozana na kamati ya uinjilisti ya Umoja huo, hivi karibuni walitembelea mtaa wa Mvuti, ambao ni mmoja ya mitaa inayotunzwa na usharika wa Azania Front Cathedral,

Ziara hiyo ya siku moja, ilikuwa na makusudi ya kwenda kushiriki ibada, ikiwa ni pamoja na kukutana na wanawake wa mtaa huo ili kujua mnaendeleo yao, pamoja  na changamoto zao,  kiroho na kiuchumi, pia viongozi hao waliweza kutembelea darasa la shule ya jumapili, ambalo umoja wa wanawake hushiriki kutoa huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya chai kwa watoto hao kila Jumapili.

Baadhi ya picha za matukio tofauti wakati wa ziara ya viongozi wa Umoja wa Wanawake katika mtaa wa Mvuti.

------------------------------------------------------------

Ripoti hii imeandaliwa na Jane Mhina