Date: 
11-07-2025
Reading: 
1 Timotheo 4:11-12

Ijumaa asubuhi tarehe11.07.2025

1 Timotheo 4:11-12
11 Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.
12 Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Msingi wa uongozi bora;
Kijana Mkristo ni chachu ya maendeleo;

Mtume Paulo anamwandikia Timotheo akimsihi kuwa  mtumishi mwema katika Kristo. Anamtaka kuifundisha kweli ya neno la Mungu kama alivyomfundisha. Yaani Paulo hataki Timotheo akae na maarifa aliyopewa peke yake, anamtaka akawafundishe wengine, maana neno la Mungu ni kwa ajili ya watu wote. Kwa hiyo Paulo kwa mamlaka ya neno la Mungu anamtuma Timotheo kuhubiri Injili 

Paulo anaendelea kumtaka Timotheo kuishi maisha yenye kumcha Bwana, katika ujana wake ili awe mfano kwa wengine. Ndiyo maana anamwambia kwamba mtu yeyote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwa waaminio katika mwenendo, upendo, imani na usafi. Timotheo anaitwa kuishi katika Bwana, nasi vivyo hivyo. Amina.
Ijumaa njema

Heri Buberwa 
Mlutheri