Date: 
11-12-2024
Reading: 
Luka 21:29-33

Hii ni Advent 

Jumatano asubuhi tarehe 11.12.2024

Luka 21:29-33

29 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote.

30 Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.

31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.

32 Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.

33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Ukombozi wetu umekaribia;

Yesu anaonesha ambavyo watu waliona mtini umechipuka na kungojea mavuno. Alitumia mfano wa mtini ambao ulikuwa katika mazingira husika. Ni kama sisi tunapoona mazao yetu yameota, mvua zikinyesha vizuri huwa tunajua mavuno yamekaribia, tukingojea mavuno kwa hamu.

Yesu alitumia mfano huu kuelezea ufalme wake, kuwa u karibu. Kuwepo kwake naweza kusema ni mazao yanaendelea vizuri shambani. Mavuno yako karibu, yaani Yesu yu karibu kurudi. 

Umejiandaaje ili anaporudi asikuache? 

Uwe na Jumatano njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri