Date: 
09-12-2024
Reading: 
Zekaria 9:14-17

Hii ni Advent 

Jumatatu asubuhi tarehe 09.12.2024

Zekaria 9:14-17

14 Naye Bwana ataonekana juu yao, Na mshale wake utatoka kama umeme; Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini.

15 Bwana wa majeshi atawalinda; Nao watakula na kuyakanyaga mawe ya teo; Nao watakunywa na kufanya kelele kama kwa divai; Nao watajazwa kama mabakuli, kama pembe za madhabahu.

16 Na Bwana, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimeta-meta juu ya nchi yake.

17 Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.

Ukombozi wetu umekaribia;

Sura ya 9 ya unabii wa Zekaria ni utabiri wa ujio wa Yesu Kristo. Yesu anatabiriwa kuja kama mfalme mwenye wokovu kwa watu wote. Inaanzia mstari wa 9 kama tunavyosoma;

Zekaria 9:9

Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.

Somo linamtaja Yesu ajaye kama mfalme mwenye wema mwingi. Huyu ndiye tunakumbushwa kumpokea, ili ajapo atupe uzima wa milele. Tujiandae kumpokea maana ukombozi wetu umekaribia. Amina

Jumatatu njema

 

Heri Buberwa 

Mlutheri