Date: 
07-12-2024
Reading: 
1Wathesalonike 5:1-5

Hii ni Advent 

Jumamosi asubuhi tarehe 07.12.2024

1 Wathesalonike 5:1-5

[1]Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

[2]Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

[3]Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

[4]Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

[5]Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

Bwana analijia Kanisa lake;

Mtume Paulo anawaandikia Wathesalonike kuwa tayari kumpokea Bwana, ambaye atakuja kama mwizi. Mwizi hatoi taarifa, huvamia ghafla! Hapa ujumbe wa Mtume Paulo ni kuwa hatujui siku wala saa Bwana atakaporudi, hivyo kujiandaa muhimu.

Ujumbe huu unakuja kwetu asubuhi ya Jumamosi hii kutukumbusha kuwa Yesu atarudi siku tusiyoijua, hivyo tuwe tayari wakati wote kumpokea. Jiandae kumpokea Bwana, siku isiyojulikana atarudi. Amina

Uwe na Jumamosi njema

 

Heri Buberwa