Date: 
05-12-2024
Reading: 
Isaya 27:1-9

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 05.12.2024

Isaya 27:1-6

[1]Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.

[2]Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.

[3]Mimi, BWANA, nalilinda, 

Nitalitia maji kila dakika, 

Asije mtu akaliharibu; 

Usiku na mchana nitalilinda.

[4]Hasira sinayo ndani yangu; 

Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, 

Ningepanga vita juu yake, 

Ningeiteketeza yote pamoja.

[5]Au azishike nguvu zangu, 

Afanye amani nami; 

Naam, afanye amani nami.

[6]Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; 

Israeli atatoa maua na kuchipuka; 

Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.

Bwana analijia Kanisa lake;

Isaya analeta tangazo la ukombozi kwa Israeli, Bwana akiahidi kuwaangamiza wote walio kinyume na Taifa lake. Hii ilikuwa ahadi ya wokovu, Mungu akiahidi kuwapigania watu wake.

Nasi Mungu hutupigania siku zote, na katika hilo ni muhimu kukaa katika wokovu aliotupa ili tuwe na mwisho mwema, maana Bwana analijia Kanisa lake. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa