Date: 
05-07-2024
Reading: 
1 Wakorintho 4:14-21

Ijumaa asubuhi tarehe 05.07.2024

1 Wakorintho 4:14-21

14 Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao.

15 Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.

16 Basi, nawasihi mnifuate mimi.

17 Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.

18 Basi wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu.

19 Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu waliojivuna, bali nguvu zao.

20 Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.

21 Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?

Ninyi ni barua ya Kristo;

Mtume Paulo anawaonya Wakorintho kuwa makini na walimu wengi walioko katikati yao. Anawakumbusha kuwa wana walimu wengi, lakini hawana baba wengi. Kwa njia hiyo anawataka kumfuata yeye. Aliwaambia hivi kwa maana ya kuenenda kwa kuiishi Injili aliyowahubiria, na siyo vinginevyo.

Kumbe Mtume Paulo alikuwa anawataka kuishi kwa kumfuata Kristo kama alivyowahubiria na kuwafundisha. Kwa muktadha wa tafakari ya Juma hili, naweza kusema Mtume Paulo aliwataka watu wa Korintho kuishi kwa neno la Mungu, maisha yao yakiwa na ushuhuda. Ndiyo wito tunaopewa leo, kwamba tuwe barua ya Kristo. Amina

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa