MATANGAZO YA USHARIKA 

LEO TAREHE 19 NOVEMBA, 2023

SIKU YA BWANA YA 2 KABLA YA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

HUKUMU YA MWISHO INAKUJA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 12/11/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii wanashukuru sana kwa kuwawezesha kufanya mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa mwaka wa Kwanza na wa pili yaliyofanyika jana jumamosi tarehe 18/11/2023 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka sa 8.00 mchana hapa Usharikani. Pia Wanashukuru Wazazi na Walezi walioweza kuhudhuria na kushiriki kujadili juu ya changamoto za Malezi ya Watoto. Mungu awabariki sana.

 6. Jumanne ijayo tarehe 21/11/2023 saa 10.30 jioni Mchungaji atakutana na Wanafunzi wa Kipaimara Mwaka wa pili Pamoja na Wazazi/Walezi mnaombwa kuhudhuria siku hiyo bila kukosa.

7. Jumamosi ijayo tarehe 25/11/2023 kutakuwa na ibada ya Ubarikio kwa watoto wa Kipaimara kwa Kiswahili. Ibada itaanza saa 3.00 asubuhi. pia jumamosi ya 02/12/2023 kutakuwa na ibada ya ubarikio kwa watoto wa Kipaimara kwa Kingereza. Ibada itaanza saa 3.00 asubuhi Washarika tuziombee ibada hizi muhimu.

8. Jumapili ijayo tarehe 26/11/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

9. SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 26/11/2023

IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI

  • Familia ya Bwana na Bibi Isaya Shekifu watamtolea Mungu shukrani ya pekee kwa mambo mengi aliyowabariki na kuwatendea.

Neno: YEREMIA 30:19. Wimbo: Mungu Amenihurumia 295 

10. NDOA ZA WASHARIKA

MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 09/12/2023 

SAA 07:00 MCHANA

  • Bw. Nguzo Heriel Kida na Bi. Catherine Ngarami Mushi 

MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 25/11/2023 

SAA 09:00 ALASIRI

  • Bw. Peres Peter Meena na Bi. Aneth Anase Monyo 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa Prof. na Bibi Mashalla
  •  
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bw na Bibi Charles Lyimo
  • Mjini kati: Watafanyia hapa usharikani saa 1.00 asubuhi
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Albert Olotu
  •  Upanga: Kwa Bwana na Bibi Munissi
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Bwigane itafanyika siku ya jumatano tarehe 22/11/2023 saa 12 jioni

12. Zamu: Zamu za wazeeni ni Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu,

Bwana ayabariki.