Date: 
20-09-2023
Reading: 
Matendo 10:1-8

Jumatano asubuhi tarehe 20.09.2023

Matendo ya Mitume 10:1-8

1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,

2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.

3 Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!

4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.

5 Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro.

6 Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda.

7 Na yule malaika aliyesema naye akiisha kuondoka, Kornelio akawaita wawili katika watumishi wake wa nyumbani, na askari mmoja, mtu mtauwa katika wale waliomhudumia daima;

8 na alipokwisha kuwaeleza mambo yote akawatuma kwenda Yafa.

Mungu hujishughulisha na maisha yetu;

Kornelio wa Kaisaria alitokewa na Bwana awatume wasaidizi wake kwenda kwa Petro. Wasaidizi wake walienda kwa Petro, wakarudi naye kwa Kornelio. Kornelio alimpokea Petro, jambo ambalo halikuwa la kawaida kwa Myahudi na asiye Myahudi kuchangamana. 

Ndipo Petro akaja na ujumbe maarufu;

Matendo ya Mitume 10:34-36

34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
36 Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),

Hadi hapa, Bwana anaonekana kuunganisha Wayahudi na wasio Wayahudi. Tafsiri yake ni kuwa Yesu Kristo ni wa watu wote. Ujumbe wa Petro kwa watu wa Kaisaria ulihusu Yesu aokoaye, asiye na upendeleo. Tudumu katika Kristo, ambaye hujishughulisha na maisha yetu. Amina.

Jumatano njema.

Heri Buberwa