Jumapili tarehe 19/10/2014, Kwaya ya upendo ilifanya ziara ya kumtembelea Chaplain Mzinga nyumbani kwake, kumjulia hali baada ya kurejea toka safari ya matibabu India. Mambo yalikua kama hivi:-
Mlezi wa kwaya, Joyce Kasyanju akiwakilisha Ua na Kadi kwa Mama Mzinga niaba ya kwaya.
Mama Shekidele, mzee wa usharika naye alikuwepo
Mwalimu wa kwaya akiwakilisha zawadi ya Tunda kwa Mama Mzinga, ambaye pia ni mwanakwaya.
Mzee Minja alitoa neno la shukrani akiwatia moyo Mama na Chaplain
________________________________________________________________
Baada ya Zawadi, Mama Apaaisaria Kilewo alifanya sala kumwombea Chaplain na familia yake, na kwaya. Ilifuatiwa na viburudisho ilivyoandaliwa na Mama Mzinga.