Date: 
01-03-2021
Reading: 
Mathayo 2:13-15

Jumatatu asubuhi; 01.03.2021

Mathayo 2:13-15

[13]Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

[14]Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;

[15]akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu.

Ukatili ni uovu;

Baada ya Mamajusi kumuona na kumsujudia mtoto Yesu, wanaelekezwa na malaika wasirudi kwa Herode, wakarudi kwa njia nyingine, maana Herode alipanga kumuua mtoto. Ndipo katika somo la leo asubuhi, malaika anamtokea Yusufu akimwambia kumpeleka mtoto Yesu Misri, ili asiuawe na Herode.

Yupo miongoni mwetu leo mwenye roho kama ya Herode? Katili, aliye tayari hata kuua kwa sababu ya maslahi binafsi? Hii haitakiwi kabisa, maana mwenye hii tabia hataiepuka ghadhabu ya Mungu. Upendo wa Mungu utawale miongoni mwetu kwa ajili ya Utukufu wake, tusiwe na roho mbaya, maana ukatili ni uovu.

Nakutakia wiki njema.


Monday 1st March 2021, Morning

Mathew 2:13-15

13 And when they were departed, behold, the angel of the Lord appeareth to Joseph in a dream, saying, Arise, and take the young child and his mother, and flee into Egypt, and be thou there until I bring thee word: for Herod will seek the young child to destroy him.

14 When he arose, he took the young child and his mother by night, and departed into Egypt:

15 And was there until the death of Herod: that it might be fulfilled which was spoken of the Lord by the prophet, saying, Out of Egypt have I called my son .

 

After the Wise Women saw and worshipped the baby Jesus, they are directed by angels not to return to Herod, and returned in other ways, meaning Herod planned to kill the child. Then in today's lesson this morning, an angel appears to Joseph telling him to take the baby Jesus to Egypt, so that he should not be put to death by Herod.

Are there among us today herod's soul-like soul? Ploting, willing to even kill because of personal interests? This is absolutely unexpectable, for this character will not escape God's wrath. God's love will dwell among us for His glory, not having evil spirits, for cruelty is evil.

I wish you a good week.