Date: 
04-11-2022
Reading: 
Marko 11:15-19

Ijumaa asubuhi tarehe 04.11.2022

Marko 11:15-19

[15]Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa;

[16]wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu.

[17]Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.

[18]Wakuu wa makuhani na waandishi wakapata habari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza; maana walimwogopa, kwa sababu mkutano wote walishangaa kwa mafundisho yake.

[19]Na kulipokuwa jioni alitoka mjini.

Ushuhuda wetu; Hapa nimesimama;

Wayahudi walikuwa na kawaida ya kuleta vitu hekaluni na kubadilishana kwa fedha, ili wasio na fedha wapate matoleo. Lakini ilifikia hatua ikawa biashara, watu wakaanza kuuziana bidhaa hekaluni. Ndipo tunasoma asubuhi hii Yesu akipindua meza zao hekaluni, akisema hekalu ni nyumba ya sala na siyo pango la wanyang'anyi.

Hekalu ni sehemu takatifu.

Yesu hakutaka lichafuliwe.

Sisi kama kundi la waaminio tunafananishwa na hekalu la Mungu, kuanzia mioyoni mwetu, maisha yetu, familia zetu na Kanisa kwa ujumla. Tukiishi maisha yasiyofaa tunakuwa sawa na waliofanya biashara hekaluni. Tukiishi kwa kumfuata Yesu tunakuwa watu wake.

Siku njema.