Date: 
14-10-2016
Reading: 
Mark 6:7-13 New International Version (NIV)

FRIDAY 14TH OCTOBER 2016 MORNING                      

Mark 6:7-13  New International Version (NIV)

Calling the Twelve to him, he began to send them out two by two and gave them authority over impure spirits.

These were his instructions: “Take nothing for the journey except a staff—no bread, no bag, no money in your belts. Wear sandals but not an extra shirt. 10 Whenever you enter a house, stay there until you leave that town. 11 And if any place will not welcome you or listen to you, leave that place and shake the dust off your feet as a testimony against them.”

12 They went out and preached that people should repent. 13 They drove out many demons and anointed many sick people with oil and healed them.

Jesus called the Apostles to follow Him and learn from Him. Here He is sending them out to do work of evangelism. Jesus is still calling people to follow Him  and to share in the work of preaching the Gospel. Perhaps you do not consider yourself to be an Evangelist or preacher but as a Christian there is something that you can do. You can share your faith with your friends and family and colleagues at work. Talk to them about Jesus and what He means to you. Invite them to church or to House to House Fellowship.     

 

 

IJUMAA TAREHE 14 OKTOBA  2016 ASUBUHI                 

Marko  6:7-13

7 Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; 
8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa fimbo tu; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni; 
9 lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili. 
10 Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale. 
11 Na mahali po pote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung'uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu, kuwa ushuhuda kwao. 
12 Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. 
13 Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza. 
 

Yesu aliwaita Mitume kumfuata na kujifunza kutoka kwake. Katika mistari hapo juu tunasikia jinsi aliwatuma kufanya Uinjilisti.

Yesu bado anaita watu kumfuata na pia kufanya uinjilisti. Labda hujasikia kama wewe ni Mwinjilisti au mhubiri lakini kuna kitu unawezakufanya. Unaweza kushuhudia marafiki, ndugu na wafanyakazi mwenzako. Uwakaribishe kanisaini au katika Ibada ya Nyumba kwa nyumba