DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 24 AGOSTI, 2025
SIKU YA BWANA YA 10 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI
HAKI HUINUA TAIFA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 17/08/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 17/08/2025 ni Washarika 773 Sunday School 241
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Uongozi wa vijana Azania unapenda kuwashukuru vijana wote walioshiriki kwenye mechi ya jumapili iliyopita tarehe 17/08/25 mchezo ulikuwa mzuri na vijana wa Azania walishinda kwa goli 3-1 dhidi ya Machimbo , Tunawapongeza vijana kwa ushindi. Jumapili ijayo tarehe 31/08/2025 watacheza mchezo wa robo fainali na Vijana wa Kinyerezi. Washarika tuendelee kuwaombea vijana wetu.
8. Ijumaa ijayo tarehe 29/08/2025 Kutakuwa na Mkesha wa maombi ya wanawake na mabinti jimbo la kati utakaofanyika Usharika wa Kariakoo kuanzia saa tatu 3.00 usiku. Wanawake na Mabinti mnaombwa kushiriki mkesha huo wa maombi bila kukosa.
9. Jumapili Ijayo tarehe 31/08/2025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.
10. Uongozi wa Usharika unapenda kuwakumbusha wazazi na walezi kuwa wale watoto tisa walioshinda mtihani ngazi ya Usharika, watakwenda kufanya mtihani ngazi ya jimbo jumamosi ijayo tarehe 30/08/2025 usharika wa Tabata. Hivyo tunaomba watoto wafike hapa Kanisani saa 1.00 ili kuanza safari ya kuelekea Tabata.
11. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 31/08/2025 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi
-
Familia ya Bwana na Bi Kenneth Zebedayo
watamshuku Mungu kwa mambo mengi ambayo Mungu amewatendea katika maisha yao ikiwa ni pamoja na: Ndoa yao kutimiza miaka 15 tarehe 15/8/2025, Mama wa familia kupona maumivu baada ya kufanyiwa operesheni, Baba wa familia kupata kazi, Watoto wao kuendelea vizuri na masomo yao mashuleni walipo.
Zaburi: 66:8-14; 19-20, wimbo: TMW 319-Yesu Unipendaye.
12. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 13.09.2025
SAA 6:00 MCHANA
-
Bw.Emanuel Joseaugusto Alexandre na Bi. Sania Martin Kasyanju
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 06.09.2025 AMBAYO ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT NJIA PANDA MOSHI KATI YA
-
Bw. Gift Godbless Mkony na Bi. Oneska James Mbwile
KWA MARA YA TATU TUNANGAZA NDOA YA TAREHE 30/08/2025
SAA 9.00 ALASIRI
-
Bw. Stuart Gamaliel Kisyombe na Bi. Paschalina Marijani Msofe
3. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Raymond Sangiwa
- Upanga: Kwa ……………………………...
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw & Bibi Frank Korassa
- Kinondoni: Kwa ………………………….
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana Kenneth Kasigila
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bibi Itemba
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Eng. Dr na Bibi Kumbwaeli Salewi
Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.