Date: 
09-11-2020
Reading: 
Mark 13:32-37

MONDAY 9TH NOVEMBER 2020 MORNING                                                      

Mark 13:32-37 New International Version (NIV)

32 “But about that day or hour no one knows, not even the angels in heaven, nor the Son, but only the Father. 33 Be on guard! Be alert[e]! You do not know when that time will come. 34 It’s like a man going away: He leaves his house and puts his servants in charge, each with their assigned task, and tells the one at the door to keep watch.

35 “Therefore keep watch because you do not know when the owner of the house will come back—whether in the evening, or at midnight, or when the rooster crows, or at dawn. 36 If he comes suddenly, do not let him find you sleeping. 37 What I say to you, I say to everyone: ‘Watch!’”

The Lord is ready to come into our hearts if the invitation that he extends is accepted. Jesus will come, however, as the Gospel indicates, when we do not expect. Therefore, we must be ready. This is the time for us to reevaluate our lives and see how we have been doing with the invitations extended by God.


JUMATATU TAREHE 9 NOVEMBA 2020 ASUBUHI                                          

MARKO 13:32-37

32 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
33 Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.
34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;
36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.
37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.

Bwana yupo tayari kuingia mioyoni mwetu ikiwa tutakubali mwaliko wake. Hata hivyo, Yesu atarudi kama Injili zinavyotuonesha, tena wakati tusiotazamia. Hivyo, ni lazima tuwe tayari. Huu ni wakati wa kujitathmini juu ya maisha yetu kuona namna ambavyo tumekuwa tukitenda juu ya mwaliko huu wa Mungu.