MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 05 JANUARI, 2025

SIKU YA BWANA YA 2 BAADA YA KUZALIWA KWA BWANA YESU KRISTO.

NENO LINALOTUONGOZA NI  

UWEZA WA MUNGU WAJIDHIHIRISHA KATIKA YESU KRISTO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 29/12/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

Mahudhurio ya ibada ya tarehe 01/01/2025 ilikuwa ni washarika 413

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Jumatatu ijayo tarehe 06/01/2025 yaani kesho saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada ya Epifania. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=. 

7. Leo tarehe 05/01/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.

8. Uongozi wa Usharika unapenda kuwataarifu Washarika wenye watoto kuanzia miaka 12 na kuendelea kuandikisha watoto kwa ajili ya darasa la Kipaimara litakaloanza mapema 2025. Fomu zinapatikana ofisi ya Parish Worker.

9. Kwaya ya AGAPE, wanatarajia kwenda kuwatembelea watoto wenye tatizo la mgongo wazi katika hospitali ya Taifa - Muhimbili, pamoja na watoto wenye uhitaji wanaolelewa katika kituo cha watoto KIBAHA CHILDREN VILLAGE CENTRE mkoa wa Pwani, January 2025. Kila mwaka kwaya ya Agape hutoa huduma hii na wanapenda kuwashukuru sana washarika wote waliojitoa kwa ajili ya huduma iliyopita. Hivyo wanaomba sana washarika kuwaunga mkono kwa kuchangia huduma hiyo. Unaweza kuchangia fedha taslimu, nguo, mafuta ya ngozi, sabuni za kufulia na kuogea, madaftari, kalamu, maji ya kunywa, dawa za meno au chochote utakachobarikiwa na Mungu. Tafadhali wasilisha sadaka yako ofisi ya Usharika au unaweza kutuma sadaka yako kupitia Account no 3874006021 jina AGAPE EVANGELICAL SINGER AZANIA FRONT Maendeleo Bank. Mungu wa Mbinguni awabariki sana.

10. SHUKRANI –Jumapili ijayo tarehe 12/01/2025 katika Ibada ya tatu Saa 4.30 Asubuhi.  

  • Familia ya Bwana na Bibi Yusuph Elieza Lazaro watamshukuru Mungu  - kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kufunga Ndoa takatifu salama hapa Azania Front tarehe 28/12/2024.

Neno: Zab. 145:1-3, Wimbo: Anza yote na Bwana toka Kwaya Kuu

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Shanny Mbogolo.

12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.