Date: 
18-07-2020
Reading: 
John 1:35-42

SATURDAY 18TH JULY 2020   MORNING                                            

John 1:35-42 New International Version (NIV)

35 The next day John was there again with two of his disciples. 36 When he saw Jesus passing by, he said, “Look, the Lamb of God!”

37 When the two disciples heard him say this, they followed Jesus. 38 Turning around, Jesus saw them following and asked, “What do you want?”

They said, “Rabbi” (which means “Teacher”), “where are you staying?”

39 “Come,” he replied, “and you will see.”

So they went and saw where he was staying, and they spent that day with him. It was about four in the afternoon.

40 Andrew, Simon Peter’s brother, was one of the two who heard what John had said and who had followed Jesus. 41 The first thing Andrew did was to find his brother Simon and tell him, “We have found the Messiah” (that is, the Christ). 42 And he brought him to Jesus.

Jesus looked at him and said, “You are Simon son of John. You will be called Cephas” (which, when translated, is Peter[g]).

 

The beauty of becoming a disciple of Jesus is that it’s not just a one-time experience. It is something that happens over and over again as our lives continue to be changed by the one who came to walk alongside us. 

Moreover, we are called to keep it going. Just as the disciples emerged from their first lesson with Jesus, eager to tell others, we, too are called to share this message. 


JUMAMOSI TAREHE 18 JULY 2020  ASUBUHI                              

 JOHN 1:35-42

35 Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.
36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!
37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.
38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?
39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
40 Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.
41 Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).
42 Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).

 

Uzuri wa kuwa mfuasi wa Yesu Kristo ni kuwa, siyo jambo linakokamilika kwa wakati mmoja. Ni jambo endelevu, na maisha yetu huendelea kubadilishwa na yeye aliyetuita na kukubali kuandamana nasi. 

Zaidi ya yote, tunaitwa kuendelea mbele. Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Yesu walipomsikia Bwana kwa mara ya kwanza, walitamani kuwaeleza wengine; sisi pia, tunaitwa kuwashuhudia wengine habari za Yesu.