Sikukuu ya Mavuno 2019

Jumapili ya tarehe 27 Oktoba 2019, ilikuwa siku ya sherehe ya mavuno hapa kanisa kuu Azaniafront ikiongozwa na msaidizi wa Askofu Mch Chidiel Lwiza akisaidiana na Chaplain Charles Mzinga. Sherehe ilianza kwa maandamano yalioongozwa na kikundi cha Tarumbeta cha Azaniafront.Washarika walipata nafasi ya kuleta mavuno yao ya fedha, mazao, mifugo, na kazi za mikono madhabahuni kwa Bwana. Pia ilikuwepo kwaya iliyoalikwa ya Mkombozi kutoka KKKT Msasani. Kwaya ya umoja ya Azaniafront ilikuwepo pia japo baadae waliondoka kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ngazi ya jimbo.