
Jumapili ya tarehe 27 Oktoba 2019, ilikuwa siku ya sherehe ya mavuno hapa kanisa kuu Azaniafront ikiongozwa na msaidizi wa Askofu Mch Chidiel Lwiza akisaidiana na Chaplain Charles Mzinga. Sherehe ilianza kwa maandamano yalioongozwa na kikundi cha Tarumbeta cha Azaniafront.Washarika walipata nafasi ya kuleta mavuno yao ya fedha, mazao, mifugo, na kazi za mikono madhabahuni kwa Bwana. Pia ilikuwepo kwaya iliyoalikwa ya Mkombozi kutoka KKKT Msasani. Kwaya ya umoja ya Azaniafront ilikuwepo pia japo baadae waliondoka kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ngazi ya jimbo.

Chaplain Chales Mzinga akiongoza maandamano.

Wazee wakanisa wakiwa kwenye maandamano


Watoto wa Shule ya Jumapili na waalimu wao walikuwepo kwenye maandamano

Baadhi ya washarika wakiingia kwa maandamano

Washarika wakiwa kwenye maandamano

Kwaya ya Mkombozi wakiimba

Wazee wa kanisa wakipokea mavuno Fedha.

Na watoto wa Shule ya Jumapili walikuwepo pia.

Juu kutoka kulia ni Dean Chidiel Lwiza, Chaplain Mzinga na Naibu Katibu wa baraza Brenda Msangi Kinemo. Chini ni Mzee wa kania Dr. Mkony wakifualilia ibada.

Baadhi ya wazee wa kanisa wakiwa wamejipanga wakati maandamano yakiingia.

Sehemu ya Kikundi cha tarumbeta katika wimbo


Dean Lwiza akihubiri

Washarika wakifuatilia ibada


Dean Lwiza akinadi picha, pembeni ni vitu vingine vililetwa kunadiwa.

