Date: 
04-11-2019
Reading: 
Revelation 17:12-18 (Ufunuo 17:12-18)

MONDAY 4TH NOVEMBER 2019  MORNING                                        

Revelation 17:12-18 New International Version (NIV)

12 “The ten horns you saw are ten kings who have not yet received a kingdom, but who for one hour will receive authority as kings along with the beast. 13 They have one purpose and will give their power and authority to the beast. 14 They will wage war against the Lamb, but the Lamb will triumph over them because he is Lord of lords and King of kings—and with him will be his called, chosen and faithful followers.”

15 Then the angel said to me, “The waters you saw, where the prostitute sits, are peoples, multitudes, nations and languages. 16 The beast and the ten horns you saw will hate the prostitute. They will bring her to ruin and leave her naked; they will eat her flesh and burn her with fire. 17 For God has put it into their hearts to accomplish his purpose by agreeing to hand over to the beast their royal authority, until God’s words are fulfilled. 18 The woman you saw is the great city that rules over the kings of the earth.”

All the inhabitants of the earth would be deceived, except the remnant of the elect. Christ must reign till all enemies are put under his feet. The reason of the victory is that he is the King of kings, and Lord of lords. He has supreme dominion and power over all things; all the powers of earth and hell are subject to his control. His followers are called to this warfare, and they will be victorious with Him.


JUMATATU TAREHE 4 NOVEMBA 2019  ASUBUHI                                 

UFUNUO 17:12-18

12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.
14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
15 Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.
16 Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.
17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.
18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.

Watu wote wa dunia watapotoshwa na yule mwovu, isipokuwa watakaosalia miongoni mwa wateule. Kristo ni lazima atawale hadi maadui wote watakapowekwa chini ya miguu yake. Sababu ya ushindi huu ni kwamba, yeye ni mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana. Anayo mamlaka na nguvu juu ya vitu vyote; nguvu zote za duniani na kuzimu zimewekwa chini yake. Wafuasi wa Kristo wanaitwa kupigana vita hii, nao watapata ushindi pamoja naye.