Juma Takatifu;
Jumamosi asubuhi 16.04.2022
Waebrania 10:1-7
1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?
3 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.
4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.
5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari;
6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;
7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu.
Aliteswa na kufa kwa ajili yetu;
Zamani watu walikombolewa kwa sheria za torati, yaani dhabihu na maelekezo mengineyo. Dhabihu hizo ziliweka Kumbukumbu ya dhambi kila mwaka. Lakini kwa kuteswa na kufa msalabani kwa Yesu Kristo, tuliokolewa kutoka dhambini.
Yesu aliteswa na kufa kutuokoa, akiondoa sadaka za kuteketezwa, kama ilivyoagiza torati. Wokovu wetu ni hakika katika Kristo. Alikuja kuyatimiza mapenzi ya Mungu, yaani kuukomboa ulimwengu na dhambi. Maisha yako yanaakisi kukombolewa?
Siku njema.