Date: 
12-03-2022
Reading: 
Waamuzi 3:1-6

Hii ni Kwaresma 

Jumamosi asubuhi tarehe 12.03.2022

Waamuzi 3:1-6

1 Basi haya ndiyo mataifa ambao Bwana aliwaacha, ili awajaribu Israeli kwa hao, yaani, awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kanaani;

2 ili kwamba vizazi vya wana wa Israeli wapate kujua ili kuwafundisha vita, hasa wao ambao hawakujua vita kabla ya wakati ule;

3 aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi.

4 Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua kwamba watasikiliza amri za Bwana, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa.

5 Basi wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao Wahiti, na hao Waamori, na hao Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi;

6 wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe wakawaoza wana wao waume, na kuitumikia miungu yao.

Tukimtegemea Bwana Tutashinda majaribu;

Somo la leo asubuhi liko katikati ya wana wa Israeli kumuasi Mungu. Ukisoma nyuma kidogo;

Waamuzi 2:20
Basi hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili wamelihalifu agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu;

Lakini tunasoma akiwajaribu kwa kuwapa nafasi ya kumrudia. Aliwapa nafasi kuona kama wangezishika amri za Bwana walizopewa kwa mkono wa Musa. Ukisoma tena kuanzia mstari wa 7, unaona hasira ya Mungu ikiwaka tena juu yao kwa sababu ya uasi wao. 

Maisha yetu yamejaa vikwazo vinavyosababisha tumkosee Mungu. Lakini Mungu anatupa nafasi ya kumrudia wakati wote. Kwa maneno mengine anatuita kutubu, na anatungojea atusamehe. 

Majira haya yatukumbushe kuwa Yesu aliteswa na kufa kwa ajili yetu, ili tuokolewe kutoka dhambini. Na leo anatuita tumrudie, tukiishi maisha yenye utukufu wake. Tunaishije maisha yenye utukufu wa Mungu? Kwa kumtegemea Mungu ili tushinde majaribu.

Jumamosi njema.