Date: 
05-11-2022
Reading: 
Tito 1:10-16

Jumamosi asubuhi tarehe 05.11.2022

Tito 1:10-16

[10]Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao.

[11]Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.

[12]Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu.

[13]Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani;

[14]wasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli.

[15]Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.

[16]Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.

Ushuhuda wetu; Hapa nimesimama;

Mtume Paulo anamwandikia Tito akiwa Krete awaambie watu wawe watii, wawe na maneno yenye maana wakifundisha vema. Anawataka watu wa Krete wasiwe waongo. Anawataka kuwa na ushuhuda mwema katika Kristo Yesu. Paulo anakazia kuwa watu wa Krete wamkiri Mungu kwa matendo, maana walimkiri lakini matendo yao yalikuwa hayafai!

Ujumbe huu unatujia Jumamosi hii ukitutaka kuwa na matendo yanayoakisi ukristo wetu. Tusiishie kumkiri Yesu kwa maneno tu. 

Ushuhuda wetu lazima uwe mzuri. Ushuhuda mzuri ni ule unaoshuhudia mema katika maisha ya Imani. Nini nafasi yako katika hili?

Jumamosi njema.