Date: 
27-11-2017
Reading: 
Revelation 1:17-20 NIV (Ufunuo 1:17-20)

MONDAY 27TH NOVEMBER 2017 MORNING                    

Revelation 1:17-20  New International Version (NIV)

17 When I saw him, I fell at his feet as though dead. Then he placed his right hand on me and said: “Do not be afraid. I am the First and the Last. 18 I am the Living One; I was dead, and now look, I am alive for ever and ever! And I hold the keys of death and Hades.

19 “Write, therefore, what you have seen, what is now and what will take place later. 20 The mystery of the seven stars that you saw in my right hand and of the seven golden lampstands is this: The seven stars are the angels[a] of the seven churches, and the seven lampstands are the seven churches.

Footnotes:

The Apostle John imprisoned on the Island of Patmos received a vision of the risen Lord Jesus.  John was overcome by the Glory of Christ. The book of Revelations contains many pictures and promises about life in heaven.

Let us prepare for Eternal Life in heaven by trusting Jesus  Christ as our Lord and Saviour and by repenting and turning from sin.

JUMATATU TAREHE 27 NOVEMBA 2017 ASUBUHI    UFUNUO WA YOHANA 1:17-20

Ufunuo wa Yohana 1:17-20

17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. 
19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo. 
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

Mtume Yohana alikuwa katika Kisiwa cha Patmo alipata maono ya Yesu Kristo katika Utukufu wake. Yohana alijinyenyekea mbele ya Yesu.

Kitabu cha Ufunuo inatoa picha nyingi na maelezo kuhusu mambo yajayo na maisha kule Mbinguni.

Tujiandae kwa ujio wa Pili wa Yesu Kristo na maisha ya milele. Tumtegemee Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wetu na tutubu na kuacha dhambi.