Jumatatu asubuhi tarehe 27.10.2025
2 Wafalme 18:1-8
1 Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea, mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia, mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.
2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na kenda katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria.
3 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, mfano wa yote aliyoyafanya Daudi, baba yake.
4 Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani
5 Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia.
6 Maana alishikamana na Bwana, hakuacha kumfuata, bali alizishika amri zake Bwana alizomwamuru Musa.
7 Naye Bwana akawa pamoja naye, kila alikokwenda alifanikiwa; tena alimwasi mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia.
8 Akawapiga Wafilisti mpaka Gaza na mipaka yake, tangu mnara wa walinzi hata mji wenye boma.
Ushuhuda wetu;
Ondoa yaliyo chukizo mbele za Mungu;
Tunaanza juma jipya tunapoadhimisha kumbukumbu ya Matengenezo ya Kanisa kwa kumsoma Hezekia aliyeanza kutawala Yuda akiwa na miaka ishirini na tano, akatawala kwa miaka ishirini na tisa. Tunasoma kwamba alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana kwa mfano wa Daudi, baba yake. Alivunja vunja vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa, akamtumaini Bwana Mungu wa Israeli.
Tunamsoma Hezekia akishikamana na Bwana na kushika amri kama ilivyoamriwa na Musa. Bwana alikuwa naye na kila alikokwenda alifanikiwa. Hezekia tunaona akifanya Matengenezo kwa kuondoa mahali pa juu, kuzibomoa nguzo, kuikata Ashera na kuvunja vipande nyoka ya shaba. Aliisafisha nyumba ya Mungu. Nasi tusafishe Roho zetu, tayari kuurithi uzima wa milele. Amina
Uwe na wiki njema yenye baraka
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
