DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 14 SEPTEMBA, 2025

SIKU YA BWANA YA 13 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI

MTENDEE MEMA JIRANI YAKO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti. Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.

3. Matoleo ya Tarehe 07/09/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 07/09/2025 ni Washarika 763 Sunday School 220

5. Tunapenda kuwa+kumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Uongozi wa Wajane na Wagane unapenda kuwashukuru Wajane na Wagane wote waliohudhuria semina iliyofanyika jana jumamosi tarehe 13/09/2025 saa 3.00 asubuhi mpaka saa 7.00 mchana hapa Kanisani Azania Front. Pia wanashukuru sana uongozi wa Usharika kwa kuwezesha semina hiyo nzuri. Mungu awabariki sana

8. NDOA: HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA

Lakini matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe

- Upanga: Kwa Mama Frida Ndosi

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Adv. Joseph na Vupe Mpuya

- Kinondoni: Kwa ………………………….

- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi

- Oysterbay/Masaki: Kwa …………………………………………..

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bibi Itemba

- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Bwigane Kaisi ,

10. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

11. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.