Date: 
24-07-2025
Reading: 
1 Yohana 5: 1-5

Alhamisi asubuhi 24.07.2025

1 Yohana 5:1-5

1 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.

2 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.

3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

Tudumu katika fundisho la Kristo;

Yohana anaandika juu ya kuushinda Ulimwengu kwa njia ya imani. Anaanza kwa kusema kuwa kila aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Yohana anaendelea kukazia kwamba kumwamini Yesu ni kumpenda kwa kulishika neno lake. Kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu kwa sababu anayo imani. 

Mstari wa tano unahitimisha kuwa mwenye kuushinda ulimwengu ni yule aaminiye kwamba Yesu ni mwana wa Mungu. Kumbe asubuhi hii tunakumbushwa kudumu katika imani kama tulivyompokea Yesu ili tuushinde ulimwengu katika yeye aliyetuita. Mwamini Yesu uokolewe. Amina

Alhamisi njema

 

Heri Buberwa 

Mlutheri