MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 06 JULAI, 2025
SIKU YA BWANA YA 3 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI
TUHURUMIANE KATIKA KRISTO
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Mageni aliyetufikia na cheti ni Joseph Jackson Mutakumwa toka Dayosisi ya Kaskazini kati Usharika wa Moshono. Amekuja kwenye matibabu.
3. Matoleo ya Tarehe 29/06/2025
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 29/06/2025 ni Washarika 894. Sunday School 190
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
6. Leo tarehe 06/07/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.
7. Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kuwashukuru vijana wote pamoja na washarika waliohudhuria mkesha ukiofanyika hapa kanisani ijumaa tarehe 04/07/2025, hakika mkesha ulikuwa mzuri na watu walibarikiwa. Aidha Sikukuu ya vijana itafanyika jumapili ijayo tarehe 13/7/2025. Hivyo ibada zote siku hiyo zitaongozwa na vijana. vijana wote mnahimizwa kushiriki, kutakuwa na mazoezi ya maandalizi ya sikukuu kila siku kuanzia Jumatano mpaka Jumamosi muda ni saa 05:00jioni. Mungu awabariki kwa utayari wenu
8. Tarehe 27/9/25 na 28/9/25 itakuwa ni sikukuu ya Mikaeli na Watoto. Hivyo tunaomba vikundi vyote vizingatie sherehe hii muhimu, ili tuweze kuwaenzi, kuwatunza na kuwatia moyo watoto wetu kwa kuwachangia chochote ili kufanikisha sikukuu hii. Mungu awabariki sana.
9. Kutakuwa na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya Mikaeli na watoto kila jumamosi. Kwa ibada ya Kingereza watafanya saa 3.00 asubuhi mpaka saa 5.00 asubuhi na ibada ya Kiswahili saa 6.00.00 Mchana mpaka saa 8.00 mchana. Wazazi na walezi mnaombwa kuwaleta watoto kwa muda uliopangwa. Mungu awabariki.
10. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 13/07/2025 katika ibada ya saa 4.30 asubuhi,
- Familia ya Bwana na Bibi Whutson Moshi watamshukuru Mungu kwa matendo makuu mengi aliyowatendea.
Neno: Zaburi 105:1-4, Wimbo: TMW 295
11. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 12/07/2025
SAA 5.30 ASUBUHI
- Bw. Traviss Tariq Adlam na Bi. Vanessa Nashera Senkoro
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Upanga: Kwa Mama Teri
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Buchanagandi
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Anord Charles Mkony
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Dr. na Bibi Rumishaeli Shoo
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.