MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 15 JUNI, 2025
NENO LINALOTUONGOZA NI
MUNGU MMOJA, BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 08/06/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 08/06/2025 ni Washarika 819.
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Jumanne ijayo tarehe 17/06/2025 saa 11.00 jioni kutakuwa na mazoezi ya Kwaya ya Umoja kwa ajili ya maandalizi ya reformation. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria pia na washarika watakaopenda kuimba kwa ajili maandalizi haya ya reformation mnakaribishwa sana.
8. Jumamosi ijayo tarehe 21/06/2025 kutakuwa na tamasha la watoto wa Sunday School litakalofanyika Usharika wa Ukonga K.K.K.T. Wazazi na Walezi mnaombwa siku hiyo kuwaleta watoto hapa kanisani saa 12.30 asubuhi. Sare ya tamasha hilo itakuwa ni Tshirt ambazo zimeandaliwa na Dayosisi, hivyo Watoto ambao bado hawajapata tshirt mnaombwa kuwaona walimu ili kuwanunulia.
9. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na Walezi kuwa mafundisho ya Kipaimara kwa lugha ya Kiswahili yamefungwa mpaka tarehe 12/07/2025.
10. NDOA. Hakuna ndoa za Washarika.
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mbwilo
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Mwl Peter na Mwl Josephine Mlagha
- Kinondoni: Kwa Profesa Geofrey Mmari.
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Mama Joyce Kasyanju
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Mama Erica Byabato.
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.