MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 27 APRILI, 2025
SIKU YA BWANA YA 1 BAADA YA PASAKA
NENO LINALOTUONGOZA NI
YESU AJIFUNUA KWETU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 20/04/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 18 - 20/04/2025 ilikuwa ni washarika 2041. Sunday School 344. Jumatatu tarehe 21/04/2025 217
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Jumanne ijayo tarehe 29/04/2025 saa 11.00 jioni kutakuwa na mazoezi ya kwaya ya Umoja kwa ajili ya maandalizi ya Kantate. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria.
8. Jumamosi ijayo tarehe 03/05/2025 kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana kutakuwa na mazoezi ya watoto wa Sunday school kwa ajili ya maandalizi ya Tamasha. Wazazi na Walezi mnaombwa kuwaleta watoto kwenye mazoezi na kufika kwa wakati.
9. Jumapili ijayo tarehe 04/05/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
10. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 04/05/2025 katika ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi.
- Mh. Mama Anna Mkapa atamshukuru Mungu kwa kumbukumbu ya kuzaliwa tarehe 29/04.
Ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi
- Mhe. Balozi Judge Mstaafu James Kateka atamshukuru Mungu kwa kumbukumbu ya kuzaliwa tarehe 29/04.
11. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 10/05/2025
SAA 7.00 MCHANA
- Bw. Gilbert Bryson Mshanga na Bi. Jacqueline Samora Kihwele
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 03/05/2025
SAA 4.00 ASUBUHI
- Bw. Eliad Augustine Mugambila na Bi. Maryness Lwessigobuta Kilenzi
NDOA IFUATAYO ITAFUNGWA PAROKIA YA MT. THOMAS MORE – MBEZI BEACH KATI YA
- Bw. Franklin Victor Lubuva na Bi. Doreen-Maria Dallas Mwanauta
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Upanga: Kwa …………………..
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Adv na Adv. Joseph Mpuya
- Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa……………………………………...
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa……………………………..
- Kawe,Mikocheni , Mbezi Beach: Kwa………………………….
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.]
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.