Date: 
24-04-2025
Reading: 
Matendo ya mitume 2:22-24

Hii ni Pasaka

Alhamisi asubuhi tarehe 24.04.2025

Matendo ya Mitume 2:22-24

22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;

23 mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;

24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.

Tembea na Yesu mfufuka;

Somo la asubuhi hii ni sehemu ya hotuba ya Petro siku ile ya Pentekoste. Petro anahutubia akisema Yesu alidhihirishwa na Mungu kwa miujiza, ajabu na ishara, lakini badala ya kuamini wale Wayahudi wakamsulibisha wakamwua. Petro anaendelea kuonesha ukuu wa Mungu kwamba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu, ili kuwaokoa wanadamu.

Hotuba ya Petro ilikuwa ndefu, na baada ya kumsikiliza walichomwa mioyo yao kama tunavyoona hapa;

Matendo ya Mitume 2:37-38

37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Watu waliamini siku ile, Kanisa likaanza kwa nguvu. Walibatizwa watu wapatao elfu tatu. Naweza kusema baada ya hotuba ya Petro waliamua kutembea na Yesu mfufuka. Wito wangu kwako asubuhi hii ni huohuo, tembea na Yesu mfufuka. Amina

Alhamisi njema

 

Heri Buberwa