MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 02 FEBRUARI, 2025
SIKU YA BWANA YA 4 KATIKA MAJIRA YA UFUNUO
NENO LINALOTUONGOZA NI
MUNGU NI MLINZI WETU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia kwa cheti: ili tuwakaribishe.
3. Matoleo ya Tarehe 26/01/2025
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 26/01/2025 ilikuwa ni washarika 742. Sunday School 89
6. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
7. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
8. Jumapili ijayo tarehe 09/02/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae. Pia siku hiyo ni siku ya ubatizo wa watoto wadogo na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.
9. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 09/02/2025 katika ibada zote tatu Umoja wa vijana wa Azania, watamshukuru Mungu kwa mema yote aliowajalia mwaka 2024 na kuingia mwaka 2025.
Neno: Zaburi 54:4
10.IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mruma
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr na Bibi David Ruhago
- Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi David Mollel
- Mjini kati: Watafanyia hapa kanisani saa 1.00 asubuhi.
- Mikocheni, Kawe na Mbezi Beach: kwa Bwana na Bibi Freeman Mbowe.
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Kelvin Matandiko
11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front.org, pia tupo Facebook na Instagram.
12.Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.