Date: 
04-11-2024
Reading: 
Marko 10:35-44

Jumatatu asubuhi tarehe 04.11.2024

Marko 10:35-44

35 Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakamwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lo lote tutakalokuomba.

36 Akawaambia, Mwataka niwafanyie nini?

37 Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako.

38 Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?

39 Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa;

40 lakini habari ya kuketi mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari.

41 Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana.

42 Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.

43 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu,

44 na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni;

Yakobo na Yohana walimwendea Yesu wakitaka awasikilize, waliomba mmoja akae kulia na mwingine kushoto kwake. Injili ya Marko huandika kwamba walikuwa na mama yao. 

Mathayo 20:20-21

20 Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.
21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

Waliamini wangemshawishi Yesu maana mama yao alikuwa ndugu na mama yake Yesu. Yesu akawaambia hawajui wanaloomba! Wale wanafunzi kumi waliobaki wakawakasirikia Yakobo na Yohana, maana walijipeleka kwa Yesu wakitaka kukaa naye peke yao. Yakobo na Yohana walitegemea wangeingia katika ufalme wa Mungu kwa kukaa pembeni mwa Yesu. Yesu akawaambia atakaye mkubwa awe mtumwa wa wenzake. Alikuwa anawafundisha unyenyekevu na kumcha ili kuingia katika ufalme wake. Tutakuwa wenyeji wa mbinguni kwa kumwamini Yesu na kuwa wanyenyekevu. Amina

Uwe na wiki njema

Heri Buberwa 

Mlutheri