Date:
22-10-2024
Reading:
1Timotheo 6:20-21
Jumanne asubuhi tarehe 22.10.2024
1 Timotheo 6:20-21
20 Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;
21 ambayo wengine wakiikiri hiyo wameikosa Imani. Neema na iwe pamoja nanyi.
Tuishindanie Imani katika Kristo Yesu;
Somo la asubuhi hii ni mwisho wa waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Timotheo, ambapo baada ya kumuandikia Timotheo akimuagiza kuhubiri na kufundisha juu ya vita vya imani, anamtaka kuilinda Imani yake. Anamtaka kujiepusha na maneno yasiyo na maana, pia anamtaka kujiepusha na elimu ya uongo.
Ujumbe tunaoupata asubuhi ya leo ni kusimama katika imani yetu kama tulivyompokea Yesu Kristo. Tuilinde imani yetu kwa kuepuka mambo yote yasiyofaa. Tunapoishi, imani yetu ituongoze kuwaza, kunena na kutenda kwa Utukufu wa Mungu, leo na siku zote. Amina
Jumanne njema
Heri Buberwa