Date: 
14-10-2024
Reading: 
Wakolosai 2:20-23

Jumatatu asubuhi tarehe 14.10.2024

Wakolosai 2:20-23

20 Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,

21 Msishike, msionje, msiguse;

2.2 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?

23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

Ni baraka kuitikia wito;

Mtume Paulo anawaonya watu wa Kolosai juu ya walimu wa uongo. Anawaambia kuwa kama walikufa na Kristo na kuyaacha mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kuyarejea tena? Paulo anasema mafundisho ya uongo yaweza kuonekana yana hekima kwa ibada za kujitungia lakini hayafai kitu katika kulisaidia Kanisa la Mungu.

Alichokiongelea Paulo kwa Wakolosai ndicho kimeshika hatamu leo, mafundisho ya uongo yamejaa kila mahali! Jambo la kusikitisha hata baadhi ya viongozi wanaruhusu walimu wa uongo kufundisha uongo wao Kanisani! Wanawapoteza waamini, yaani kuwafanya waamini kama vile hawajawahi kusikia Injili, maana kinachofundishwa ni tofauti na neema ya Mungu. Tunaitwa kuyaepuka mafundisho ya uongo. Tusiyape nafasi. Kweli ya Kristo ituweke huru daima. Amina

Uwe na wiki njema

Heri Buberwa