Date: 
04-09-2024
Reading: 
Waefeso 4:25-29

Jumatano asubuhi tarehe 04.09.2024

Waefeso 4:25-29

25 Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.

26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;

27 wala msimpe Ibilisi nafasi.

28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.

29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Mpende Jirani yako;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Efeso kuwa na maisha mapya katika Kristo (4:17-24). Anawaita kuvaa utu upya ulioumbwa kwa namna ya Mungu. Tusome kwa ufupi;

Waefeso 4:22-24

22 mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;
23 na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;
24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

Somo la asubuhi hii ni mwendelezo wa maisha mapya, Paulo akisisitiza juu ya kuacha uongo na kusema kweli kwa kila mtu na jirani . Paulo anaendelea kusema kwamba wawe na hasira, lakini wasitende dhambi, jua lisichwe uchungu ukiwepo. Mwizi aache kuiba, afanye kazi kwa bidii.  

Ujumbe wa Mtume Paulo ni kwa waaminio kuwa na maisha mapya katika Kristo wakiishi vizuri na majirani zao. Nasi tuishi vizuri na jirani zetu. Mpende jirani yako kama nafsi yako. Amina

Jumatano njema

Heri Buberwa