Date: 
15-07-2024
Reading: 
Wafilipi 2:3-4

Jumatatu asubuhi tarehe 15.07.2024

Wafilipi 2:3-4

3 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.

4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Wito wa kuwajali wengine katika Kristo;

Mtume Paulo anawaandikia Wafilipi kuwa na nia moja katika Kristo. Katika kukazia hilo, anawataka kutotenda jambo lolote kwa kujivuna wala kushindana, bali kwa unyenyekevu kila mmoja akimuona mwenzake bora kuliko yeye. Katika kuwa pamoja na kusaidiana, Paulo anawaambia Wafilipi kwamba kila mmoja aangalie mambo ya wengine.

Andiko la Paulo ni gumu sana kutekelezeka pasipo msaada wa Mungu. Yaani kumuona mwenzako bora kuliko wewe? Kuwa na nia moja, yaani kutenda kazi kwa pamoja? Kwamba uangalie kazi za wengine kwa nia njema? Ni vigumu sana maana sisi wengi tu wabinafsi. Lakini Yesu anatufundisha kuwajali wengine katika yeye, tukikaa pamoja kwa upendo utokao kwake. Inawezekana kwa neema ya Mungu. Amina.

Jumatatu njema.

Heri Buberwa