Jumamosi asubuhi tarehe 27.08.2024
Marko 2:18-22
18 Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
19 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga.
20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile.
21 Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipotatuka huzidi.
22 Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya.
Maisha mapya ndani ya Kristo;
Wafuasi wa Yohana na wale wa Mafarisayo walikuwa wakifunga. Hawa walikuwa wakifunga kama sehemu ya maombolezo na toba kwa ajili ya Taifa lao. Hapa ni muhimu kukumbuka kuwa Yohana alikuwa gerezani, hivyo inawezekana walifunga na kusali ili Yohana aachiwe kutoka gerezani.
Yesu anawaeleza kuwa yeye ndiye Mesiya. Kwa maelezo ya Yesu, siyo sahihi kuomboleza kwa uwepo wa Mesiya. Yaani wanafunzi wa Yohana na wale wa Mafarisayo hawakutakiwa kuhangaika tena, maana tayari walikuwa na Yesu. Wokovu tuliopewa na Kristo unatosha kutupa maisha mapya katika yeye. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa