Date: 
04-03-2024
Reading: 
Zaburi 91:11-16

Hii ni Kwaresma 

Jumatatu asubuhi tarehe 04.03.2024

Zaburi 91:11-16

11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.

15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;

16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

Tumtazame Bwana aliye tumaini letu;

Zaburi ya 91 huelezea jinsi waamini waishio maisha ya ushirika na Mungu walivyo salama chini ya ulinzi wake. Ukisoma kuanzia mstari wa kwanza unamuona mtu anayekaa chini ya uvuli wa Mwenyezi, ambaye amemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. 

Sasa ukiangalia somo la asubuhi hii, ndipo unaona kwamba malaika wa Bwana ataagizwa kumlinda yeye amtegemeaye Bwana. Atawaseta kwa miguu nyoka na Simba kwa msaada wa Bwana. Hivyo tunaona kuwa Zaburi hii huahidi yeyote amtegemeaye Bwana kuwa chini ya ulinzi wake. 

Ahadi ya ulinzi wa Mungu haimaanishi kutokutana na hatari, bali katika hatari zozote, kuwa salama katika Bwana. Zaburi hii imekuwa faraja kwa waaminio kwa miaka takribani 3,000, sasa iendelee kuwa faraja kwetu pia. Kwamba tumtazame Bwana wakati wote aliye tumaini letu, maana yeye hututunza daima. Amina.

Uwe na wiki njema.

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650