Date: 
04-12-2023
Reading: 
Yeremia 33:14-16

Hii ni Advent 

Jumatatu asubuhi tarehe 04.12.2023

Yeremia 33:14-16

14 Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapolitimiza neno lile jema nililolinena, katika habari za nyumba ya Israeli, na katika habari za nyumba ya Yuda.

15 Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii.

16 Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.

Bwana analijia Kanisa lake;

Yeremia alitumwa na Mungu kutoa unabii kwa Taifa lake (Mungu) juu ya ahadi yake ya ukombozi. Mstari wa 14 unalionesha hili kwa Bwana kusema kuwa atalitimiza neno lake katika nyumba ya Israeli, na katika habari za nyumba ya Yuda. Ufalme wa Daudi unaahidiwa kudumu, lakini ukifanya hukumu za haki. Yeremia anakazia kuwa Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama.

Tunachokiona asubuhi hii ni ahadi ya ukombozi kwa Israeli toka kwa Mungu. Hatimaye ahadi hii ilitimia kwa njia ya Yesu Kristo alipokuja akazaliwa kama mwanadamu, akafa na kufufuka kuukomboa Ulimwengu. Atarudi tena katika utukufu kulichukua Kanisa. Jiandae kumpokea. Amina.

Uwe na wiki njema 

Heri Buberwa