Date: 
10-11-2023
Reading: 
Mathayo 5:7-8

Ijumaa asubuhi tarehe 10.11.2023

Mathayo 5:7-8

7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Uenyeji wa mbinguni;

Ni hotuba ya mlimani inaendelea ambapo Yesu anafundisha kuhusu "Heri". Asubuhi ya leo tunasoma juu ya wenye rehema kupata rehema, na wenye moyo safi kumwona Mungu. Kama tulivyoona jana asubuhi, Yesu katika hotuba ya mlimani alikuwa anafundisha jinsi impasavyo aaminiye kuishi katika njia ya ufuasi. Mistari ya leo asubuhi kwa sehemu inatukumbusha kuwa tukirehemiwa na Bwana, tutaipata rehema idumuyo. Na mioyo yetu ikiwa safi tutamuona Mungu.

Kuishi katika rehema ni kuwa na maisha ya toba mbele za Mungu. Ni maisha ya kumtegemea Mungu wakati wote, ambapo neema ya Mungu huwa tegemeo kwa aaminiye. Moyo safi ni ule umngojeao Bwana kuurithi uzima wa milele. Mtegemee Bwana siku zote ili uwe na mwisho mwema. Amina.

Ijumaa njema.

Heri Buberwa