Date: 
09-11-2023
Reading: 
Mathayo 5:4-6

Alhamisi asubuhi tarehe 09.11.2023

Mathayo 5:4-6

4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.

5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.

6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

Uenyeji wa mbinguni;

Leo asubuhi tunasoma sehemu ya "Heri" alizozisema Yesu alipokuwa akifundisha makutano wakati wa hotuba ya mlimani. Ni hotuba ambayo ilisheheni ni kwa jinsi gani mwanadamu amfuate Kristo, yaani aishi vipi ili aingie katika ufalme wa Mungu. Leo tumesoma Yesu akisema Heri wenye huzuni, watafarijika. Wenye upole watairithi nchi, wenye njaa na kiu ya haki watashibishwa.

Wote wanaotajwa katika somo tulivyoona, yaani wenye kiu, njaa na upole, ni wale wanaomfuata Kristo katika hali yoyote. Ikibidi wanajinyima katika Bwana ili wasitoke katika kusudi la Mungu, yaani hawaiachi wala kuikana imani hadi mwisho. Usiiache imani yako hata mwisho. Amina.

Alhamisi njema 

Heri Buberwa