Date: 
08-11-2023
Reading: 
Ufunuo wa Yohana 13:14

Jumatano asubuhi tarehe 08.11.2023

Ufunuo wa Yohana 14:13 

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Uenyeji wa mbinguni;

Mstari tunaousoma leo asubuhi umezoeleka kusikika mara zote katika Liturjia ya ibada ya maziko. Hutukumbusha waumini kuishi katika Bwana, ili mwisho wetu uwe katika Bwana. Mstari huu hutukumbusha kutenda yote kwa utukufu wa Mungu maana matendo yetu huambatana nasi mara tunapotwaliwa katika maisha haya.

Yohana alifunuliwa mbingu wanayoingia wanadamu walioishi katika Bwana, ambao walikuwa na mwisho mwema maana matendo yao yaliambatana nao. Ufunuo huu unakuja kwetu asubuhi hii kutukumbusha kuishi katika Bwana, ili tufe katika Bwana. Amina.

Jumatano njema 

 

Heri Buberwa