Date: 
23-09-2023
Reading: 
2 wafalme 4:38-41

Jumamosi asubuhi tarehe 23.09.2023

2 Wafalme 4:38-41

38 Elisha akafika Gilgali tena; na kulikuwa na njaa katika nchi; na hao wana wa manabii walikuwa wakikaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, Teleka sufuria kubwa, uwapikie wana wa manabii.

39 Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu, akayachuma matango-mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasua-pasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua.

40 Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula.

41 Lakini yeye akasema, Leteni unga. Naye akautupa ndani ya sufuria; akasema, Wapakulie watu, ili wale. Wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani.

Mungu hujishughulisha na maisha yetu;

Elisha baada ya kuomba kwa Bwana, mtoto wa mwanamke mshunami aliyekufa alifufuka (1-37).

Somo letu ndipo linakuja kusema Elisha akafika Gilgali tena, nchi ambayo ilikuwa na njaa wakati ule. Elisha aliwaagiza watumishi wake kuwapikia watu chakula. Yalipikwa matango mwitu ambayo watu walishindwa kula.

Elisha aliwaambia walete unga, walipouleta akautupa kwenye sufuria, tayari ikawa chakula! Ukiendelea kusoma unaona Elisha akiletewa mikate mitano ya shayiri na masuke mabichi, chakula ambacho kilikuwa kidogo, lakini Elisha aliamuru watu wapewe, wakala na kusaza.

Soma hapa;

2 Wafalme 4:42-44

42 Tena, akaja mtu kutoka Baal-shalisha, akamletea mtu wa Mungu chakula cha malimbuko, mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani. Akasema, Uwape watu, ili wale.
43 Na mtumishi wake akasema, Je! Niwaandikie hiki watu mia? Lakini akasema, Uwape watu, ili wale; kwa kuwa Bwana asema hivi, Watakula na kusaza.
44 Basi akawaandikia, nao wakala, wakasaza, sawasawa na neno la Bwana.

Mungu alimuongoza Elisha kuwapa watu chakula katika nchi iliyokuwa na njaa. Hii inaonesha Mungu kujali watu wake. Hakuishia hapo, aliendelea kuwajali watu wake kwa kumtuma Yesu afe na kufufuka kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu. Hii ndiyo kweli, kwamba Yesu ndiye mwokozi wa Ulimwengu, ambaye hujishughulisha na maisha yetu. Dumu katika yeye (Kristo) maisha yako yote. Amina.

Jumamosi njema.

Heri Buberwa