Date: 
12-08-2023
Reading: 
Yakobo 4:13-17

Jumamosi asubuhi 12.08.2023

Yakobo 4:13-17

13 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;

14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.

15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.

16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.

17 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Tuenende kwa hekima;

Yakobo anaandika juu ya watu waishio wanavyotaka wakifikiri mafanikio yao ni kwa nguvu na maarifa yao. Watu hawa hudhani kuwa pia wanayo hatma ya maisha yao. Yakobo anasema wao ni mvuke tu, wanatakiwa kumtegemea Bwana. Yakobo anahitimisha kuwa kujisifu ni kubaya, bali kutenda mema ndilo jawabu la mambo yote.

Ujumbe wa Yakobo uko kwenye mstari wa 15, kwamba tunaweza na kutenda yote kwa mapenzi ya Mungu. Kujisifu kwa mafanikio yetu ni kukosa hekima itokayo kwa Mungu, maana Mungu ndiye hutuwezesha. Tumtegemee Mungu tukitenda mema daima. Amina.

Jumamosi njema 

Heri Buberwa